Edit Content
Click on the Edit Content button to edit/add the content.

Ninaimani mpo njema.Ningependa kuchukua muda huu kushare juu ya mfumo wa kisasa wa masoko wa *digital marketing*.Mfumo ambao unaaminika kila mfanyabiashara anahitaji kuufahamu katika karne hii ya teknolojia.Haijalishi unauza bidhaa au unatoa huduma hizi ZA *UTALII* zote zinahitaji kufanyiwa masoko ili ziweze kuwafikia wateja.

Kutokana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia na mifumo mingi kuhitaji kuendana na mabadiliko haya ya kiteknolojia nataka tuangalie ni namna gani mfumo wa biashara na masoko nao unahitaji kutoka katika mfumo uliozoeleka wa masoko na kuingia katika mfumo wa digital marketing.

Kabla ya yote ningeomba niweke angalizo kidogo watu wengi wamekuwa wakitafsiri vibaya *digital marketing* kama ni kutumia account zetu za *mitandao ya kijamii na kupost biashara zetu*.Nikiongelea *digital marketing sizungumzii kupost biashara kwenye kurasa zetu binafsi za mitandao ya kijamii au status za whatsapp* maana hiyo itabaki kuwa ni kushare tu kwa watu wako wa karibu na kupata tu pongezi kutoka kwa ndugu na jamaa zako ambao mara nyingi huwa sio wateja wa mara kwa mara.

Ninachotaka kuzungumzia hapa ni namna utakayoweza *kuwafikia wahitaji wa bidhaa au huduma zako popote walipo hata kama hufahamiani nao* (Si tafsiri rasmi ila ninajaribu kuweka maneno marahisi kwa kadiri itakavyoweza kueleweka) ningependa hii ndio iwe point kuu ya mada ya leo kwenye group letu.

Inawezekana kabisa post hii ikabadilisha mtazamo wako juu ya namna ya kutumia digital marketing katika biashara yako yako ya utalii aidha uwe mfanyabishara mdogo,au wa kati.

Kutangaza  biashara ya utalii ni moja ya muhimili mkubwa wa maendeleo ya biashara yako.Na kutokutangaza biashara limekuwa ni kosa kubwa sana la wafanyabiashara wengi wa utalii.Wengi wao wamekuwa wakidharau suala la advertising (matangazo) na kuridhika na wateja wachache wanaowafahamu waliowahi kusafiri nao kipindi cha nyuma.

“The Business That Can Spend The Most To Acquire A CustomerWins” Dan Kennedy huyu ni mshauri maarufu wa masuala ya biashara

Hapo anamaanisha biashara yoyote itakayojidhatiti kugharamia suala la kumnasa mteja basi itafanikiwa.

Haijalishi una packages nzuri za safari au huduma bora kiasi gani bila matangazo biashara yako itakuwa ni yenye kusua sua tu katika ukuaji na kuendelea.
Suala la matangazo limekuwa likiwatia hofu wafanyabiashara wengi wa utalii kutokana na gharama za matangazo kuwa kubwa na wengi wa wafanyabiashara wakihofia kutoweza kurudisha gharama hizo walizotumia katika matangazo.

Wafanyabiashara wengi wemekuwa wakitengeneza account zao katika mitandao ya kijamii na kutumia kama njia ya kunasa wateja.Ni njia nzuri sana ijapokuwa itakuhitaji utumie nguvu kubwa sana ya kushare content kwa wale wachache wanaokufahamu ili baadaye uweze kufanya nao biashara.

Njia hii sio matumizi effective ya digital marketing na teknolojia katika biashara.Kwa mtu aliye serious na biashara yake anahitaji kuwa na *online presence*.Hapa namaanisha uwe na *website yenye kuonesha huduma unazotoa* ambayo itaonesha bidhaa zote ulizonazo hapa huhitaji kuhofia ushindani kwani mamilioni ya watu wanaozunguka mitandaoni wanapofika kwenye website yako ndio kafika dukani/ofisini kwako kazi yako ni kumhudumia.

*website* ya bei nafuu na yenye ubora gharama zake haziwezi kuzidi 1,500,000 kwa malipo ya mara moja tu ambapo huhitaji malipo ya kila mwezi bali ni gharama ndogo tu za kulipia kila mwaka zisizozidi 300,000 kwa mwaka.*Acha na website za laki 3 au laki 2 za ma developer waongo ambazo zita kukost huko baadae , In reference nimekutana na wateja ambao ametengeneza website zaidi ya nne na kila website alitengenezewa kwa bei ya laki 4 na hapo kaja kwangu.*

Jaribu kufanya uchunguzi kwa kugoogle au kuingia katika mitandao ya kijamii na kuangalia ni wangapi kati ya wafanyabiashara ambao wanafanya biashara ya utalii kama wanamiliki website ya kutangaza huduma zao. Utagundua ni fursa kwako kuliteka soko mapema iwezekanavyo kabla washindani wako hawajashtuka. (WENGI WAO WANAJIITA NI MA KAMPUNI YA UTALII NA HAWANA WEBSITE WANATUMIA TU FACEBOOKS)

Jambo lingine baada ya kuwa na website ni *kutangaza biashara yako*.
Napia faida kubwa ya digital marketing inayoipiku njia tuliyozoea ya marketing ni ultra targeting.

Nini maana ya ultra targeting?

Hii ni namna ya kuchagua ni watu gani wenye rika gani na wanaotoka eneo gani wa kuwaonesha tangazo lako ili kuweza kuokoa pesa za matangazo. Unaweza kuweka tangazo na kutaka lionekane kwa jinsia fulani tu au umri fulani tu au watu wa eneo fulani tu.

Nahisi nimeandika mengi japokuwa kuna maeneo ninaweza kuwa sijayagusa kwa kiasi fulani naamini wapo wadau wengine watakaokuja kuongezea.

Najua wengi wetu ni wageni wa masuala haya ya mitandao na digital marketing hii inawafanya wasiweze kutumia fursa hii adhimu ya teknolojia.

Ikiwa wewe ni miongoni kati yao nakukaribisha sana kwa ushauri na hata msaada wa namna ya kufungua na kuanzisha online business na kutumia fursa hii ya teknolojia kukuza na kuendeleza biashara yako ya sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *